send link to app

Leoleo


4.6 ( 1456 ratings )
Biznes Żywność i napoje
Desenvolvedor: SWEETBERT DAVID
Darmowy

Bidhaa za kilimo zina sifa tofauti kidogo na bidhaa nyingine kwenye biashara. Mazao ya kilimo hubadilika katika kigezo cha wingi(idadi/upatikanaji) na bei kwa kiasi kikubwa na kwa haraka ukilinganisha na mazao mengine. Hii inafanya kuwepo kwa mabadiliko ya bei kulingana na misimu. Mf. Kipindi cha mavuno; bei za mazao mengi zinashuka na kipindi cha kuelekea msimu wa pili bei zinakua juu. Hivyo katika kuandaa mpango biashara wako ambao ndio kielelezo/dira inayokuongoza kujua namna gani na kwa kiasi gani utapata faida; ni lazima ufahamu misimu na wakati ambao bei zinapanda na kushuka ili ujue namna ya kuendesha biashara yako kwa faida. KUMBUKA UKIUZA BIDHAA KWA BEI NZURI, UNATENGENEZA MAZINGIRA YA KUPATA FAIDA ZAIDI.

TUNAKUPA TAARIFA ZA MUHIMU ZA WATEJA WAKO
Taarifa za wateja zikiwemo
1. Mahali walipo kutoka kwenye kituo cha biashara yako
2. Kiwango cha uhitaji wa bidhaa
3. Mabadiliko ya bei za bidhaa zinazofanana na zako katika soko lako
4. Mabadiliko ya mahitaji au mtazamo wa walaji wa bidhaa.

UTAFITI WA SOKO NI MSAADA WA FEDHA YAKO UNAYOTAKA KUWEKEZA KUIZUIA ISIPOPOTEE BILA KUKUINGIZIA FAIDA KWA KUWA BIASHARA NI WANUNUZI, NA WANUNUZI WAKO SOKONI.

Mabadiliko ya kupanda au kushuka kwa bei za mazao katika soko husika humpa fursa mkulima na mfanyabiashara kutambua eneo sahihi na kwa wakati husika wa kupeleka mazao yake kwaajiri ya kuuza kwa bei ya faida.
Baada ya mkulima kufanya utafiti wa kugundua mazao ambayo kwa kipindi hicho akilima anaweza uza kwa faida, hatumuachi mkulima pekeyake wakati wa kulima tunakuwa nae bega kwa bega kwa kumpatia kalenda za namna ya kulima zao hilo kupitia application yetu
na kingine tunamsaidia mkulima kupata utabiri wa bei ya baadae na hili limewezekana kutokana na wingi wa taarifa za masoko mbalimbali na wakulima wa zao hilo kwa maeneo mbalimbali.

LEOLEO GULIOSMART aplikesheni inamsaidia mkulima kufanya utafiti kabla hajaanza kulima, kutangaza au kutafta soko la mazao yake katika masoko baada ya kuvuna mazao yake kwa kuona list ya masoko katika kila mkoa na wilaya, kufahamu bei ya leo bidhaa sokoni katika masoko hayo, kuona upungufu na uhitaji wa mazao katika soko husika, hivyo kumfanya mkulima awe na uwanja mpana wa kuamua wapi aende akauze mazao yake au kupata wanunuzi katika soko gani na kwa bei gani, lakini pia kuwapatia wafanyabiashara wa mazao ya chakula fursa za mazao yanayopatikana katiaka maeneo mbalimbali shambani ambako wao wanaweza kufika na kuchukua mzao na kuja kuyauza sokoni kwa wananchi na kupata faida kwani watauza katika masoko yenye uhitaji wa zao hilo. Watumiaji wa mwisho wa mazao ya chakula (familia), wakulima na wafanya biashara wataweza kufahamu mwenendo na utabiri wa bei za mazao pamoja na kufahamu kitu gani kinahitajika sana au ambacho hakipatikani kwa wingi katika soko na masoko mengine Tanzania.